April 15, 2019


Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema kuwa klabu hiyo huenda ikawauza wacheza muhimu mwisho wa msimu huu.

Raia huyo wa Ufaransa anataka kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake baada ya msururu wa matokeo mabaya msimu huu.. (Sky Sports)

Manchester United hawana hamu na mshambuliaji wa zamani wa Lyon Moussa Dembele.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amefunga magoli 18 katika mashindano yote msimu huu. (Mirror)

Arsenal wanataka kumsaini beki wa Tottenham na Ubelgiji Toby Alderweireld, 30. (Talksport)

Mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi anatarajiwa kuondoka Inter Milan msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 huenda akahamia Real Madrid kwa dau la £52m. (AS)

Mchezaji anayelengwa na Liverpool na Bayern Munich Timo Werner hatotia saini kandarasi mpya na klabu ya RB Leipzig.

Kandarasi ya mshambuliaji huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 23 katika klabu hiyo ya Bundesliga inakamilika mwisho wa msimu huu. (Sky Germany)

Chelsea itashindana na Real Madrid katika mbio za kumnunua ,mshambuliaji wa Borussia Dortmund 19 na Sweden Alexander Isak. (Sun)

Hatahivyo Zidane mwenye umri wa miaka 46 amepinga madai kwamba atamuuza mshambuliaji wa Ufaransa Karim Benzema, 31. (Marca)

Na timu hiyo itamuuza beki wa Ufaransa Raphael Varane, 25, kwa dau la £437m kutokana na sheria inayomzuia katika kandarasi yake . (RAI Sport via Calciomercato)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic