BAADA YA KUTOLEWA CAF, SIMBA YATOA NENO ZITO KWA KLABU, YANGA WATAJWA KIAINA
Simba Simba Simba,kama ilivyo desturi yangu nnapoandika kitu SIRIAZI hutumia Tanakudi tatu kwa msisitizo!!
Yes. Wanasimba wote kuanzia viongozi,wanachama,wachezaji,benchi la ufundi na washabiki wetu wapendwa nyie ni washindi!!
Mlikuwa na lengo la kufikia Group stage halaf mkalivuka!
Mmeweka heshma ya kumaliza ligi hii ngumu ya mabingwa watupu bila kufungwa hata mechi moja nyumbani,mmejitangaza kote Afrika na mlibaki timu nane tu ktk kundi la timu zaidi ya laki moja zilizotapakaa kote barani Afrika!!
Na hakika yenu nyie ndio mtakuwa mabingwa tena wa nchi hii msimu huu,so mtarudi tena next season na nnamiini mtarudi kwa nguvu kubwa!!
Guys waacheni wanaowatania leo ila msijadiliane nao coz kujadiliana nao kuhusu ligi hii kubwa ni sawa na kumwelekeza Mtoto mchanga raha ya tendo la ndoa!!
Kalijulia wapi na yeye yake nepi?
Na Haji S Manara
Zahera kihiyo....soma hiyooo
ReplyDeleteAACHE KUITAJA YANGA ABAKI AKISHUGHULIKA NA HABARI ZA SIMBA YAKE KAMA ATAWEZA!!!
ReplyDeleteBILA KUITAJA YANGA HUNA KIKI BRO !!
MMEFUNGWA NA MAZEMBE SASA YANGA YAWAHUSU NINI HAPO !!
Wapi kaitaja Yanga!Jiwe imetupwa gizani ukitoa mguno shauri yako.
ReplyDeleteZahera ndio mpe huo ushauri kwani yeye kila akifungua mdomo Simba utafikiri ni kocha wa Simba.
Zahera anahojiwa na media kuhusu Simba anajibu kuhusu Simba ulitaka aulizwe Simba ajibu Yanga mbona uelewa wako mdogo sana
DeleteSareh acha kuandika ujinga wa MANARA kama umekosa habari tafuta kazi nyingine za kufanya, hata udobi ni kazi bro. Kazi ya habari imekushinda una copy na ku paste ujinga.
ReplyDeleteMbona akihojiwa Aussems hataji timu nyingine?Makocha wote wenye uweledi hasa wa nje,hukuti akizungumzia timu zingine.
ReplyDeleteLabda waandishi hawana cha kuuliza kuhusu Yanga?Waulize kuhusu michango?
Kocha anatakiwa azungumzie timu yake full stop.
Mhh aliulizwa onaonaje mchezo wa Mazembe na Simba???? Akajibu anavyoona yeye ulitaka ajibu nini???? Akikataa kujibu maneno yanakua mengi wabongo bana shida tupu
DeleteAussems kahojiwa lini kuhusu Yanga????? Ongea facts sio ushabiki
DeleteWakatazeni Waandishi, wasimuulize Zahera habari za Simba sio kutoa mapovu tu,Yeye siyo kichaa aulizwa habari za yanga halafu aseme simba, Msipotoshe watu
DeleteHata akihojiwa kuhusu Simba angejibu mimi sio kocha wa Simba!
ReplyDeleteAmekuwa mropokaji kwenye kila kitu.
Silence is gold .
Simba ndio habari.Migongo wazi waandishi wamechoka. Kila mara migogoro,timu haina viongozi. Kocha dikteta. Leo anamfukuza Ajibu kesho anamuita. Kwanini Ajibu asiringe?Wataripoti michango,wachezaji kukimbia njaa!
ReplyDeleteKwa Mtu mwenye busara lugha ya matusi ni udhaifu...Manara,Manara,Manara,Jiheshimu kwanza ndipo Utafute heshima kwa wengine,usiwe na mihemko mpira ndivyo ulivyo.LUGHA CHAFU YA NINI HAPA????.Tafakari ulikosea wapi urekebishe,Kutukana siyo jadi ya Watanzania,Utani upo na utaendelea kuwepo hata utoe MAPOVU Kiasi gani,..TP MAZEMBE siyo Tanzania.
ReplyDeleteWapi katukana,?Roho mbaya mmezoea hata linalowafaidi mnapinga.
ReplyDeleteKuchagua viongozi mnashindwa inabidi msimamiwe kama mna nepi!
Lakini kwa husda na majungu mna ubingwa wa dunia.
Toeni boriti kwenye jicho lenu kabla hamjazungumzia ubanzi kwenye jicho la jirani.
Migongo wazi. Michango ya TASAF inaendeleaje?
ReplyDeleteTatizo hapa co yanga bali why hatushindi ugenini? Tusijivunie kutofungwa dar tujiulize kp kgumu ugenini kila wakituona wanatuogesha?
ReplyDelete