WAKILI wa serikali, Batilda Mushi ameiambia mahakama kuwa bado hawajakamilisha upelelezi wa kesi ya Michael Wambura na kwa sasa bado wanapitia nyaraka tofauti za kesi hiyo.
Wambura anakabiliwa na mashitaka 17 likiwepo lile la utakatishaji wa fedha na kughushi nyaraka akiwa mfanyakazi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Wakili wa serikali aliiambia mahakama kuwa kwenye upelelezi wao kwa sasa unaendelea na wapo kupitia nyaraka tofauti ambazo kwa sasa hawezi kusema ni zipi.
Hata hivyo wakili wa mshitakiwa, Majura Magafu aliiambia mahakama kuwa serikali wanapaswa kuharakisha upelelezi na ili waweze kufahamu kesi yao ni ya status gani.
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mkazi Kisutu, Kelvin Mhina alisema kuwa upelelezi unatakiwa kufanyika mapema ili kesi hiyo ianze kusikilizwa.
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Aprili 25, mwaka huu ambapo itaendelea kusikilizwa na mtuhumiwa ataendelea kubaki ndani kutokana na kutokuwa na dhamana.
0 COMMENTS:
Post a Comment