April 30, 2019



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amesema kuwa ameboreka na kitendo cha timu ya Taifa ya Vijana, Serengeti Boys kufungwa mabao mengi katika ardhi ya nyumbani.

Akizungumza leo wakati wa hotuba mbele ya wananchi wa mkoa wa Mbeya wilayani Kyela ambapo yupo kwenye ziara ya kikazi, Magufuli amesema hajafurahishwa na timu ya vijana kufungwa mabao mengi uwanja wa nyumbani.

"Mashindano tumeaandaa wenyewe, uwanja wa kwetu wenyewe, tumefungwa mabao mengi kwelikweli, hili ni jambo la ajabu, tupo watu zaidi ya milioni tano na utashangaa tumefungwa na timu ambayo ina watu chini ya milioni 5, bora ungechukua timu ya Kyela naamini isingefungwa.

"Sasa hili linapaswa liangaliwe kwa usawa, ninatamani siku moja niwe Waziri wa Michezo na nikiwa Waziri wa Michezo timu nitaipanga mwenyewe, kwa hili la kupigwapigwa kwa timu yetu ya Taifa mnaniboa kweli na sijui timu ya wakubwa nayo itakwenda kufungwa? ila sio mbaya huenda kufungwa fungwa nako ni vizuri," amesema Magufuli.

Michuano ya Afcon ambayo imemalizika wikiendi hii, Cameroon imebebwa ubingwa kwa vijana, huku Tanzania ikitolewa na zigo la mabao 12 ya kufungwa na imefunga mabao sita pekee kwenye michezo mitatu.

1 COMMENTS:

  1. Tatizo la mpira wetu lipo zaidi kwa wanaosimamia mpira,namaanisha chama cha mpira Tanzania TFF.Mpira wa miguu ni siriaz business Duniani lakini kwa bahati mbaya sana viongozi wetu wanaosimamia mchezo huo bado hawana uwezo wa kusimamia ipasavyo maendeleo ya mchezo huo kumechi na ushindani wa kiutawala kutoka mataifa mengine ya Africa na Duniani kwa ujumla. Taabu sana kwa viongozi wa michezo na mpira wa miguu nchini kumuelewa nini Magufuli anataka. Muheshimiwa raisi Magufuli ni mshindani anaeamini kushinda na ni mtu anaepambana kuwaondoshea watanzania nadharia potofu ya eti sisi watanzania ni wanyonge.Inawezekana watanzania ni wanyonge lakini unyonge wetu zaidi upo kwenye akili zetu na hapo ndipo hasa panapomliza na kuutesa moyo wa Muheshimiwa raisi. Ukiangalia ndani ya kipindi cha miaka takribani minne ya uraisi wa Magufuli moja ya kazi kubwa aliyoifanya ni kuwaelimisha watanzania kuwa na hali ya kujiamini yakuwa wana uwezo tena mkubwa sana wa kufanya chochote kile cha maendeleo kama watu wa mataifa mengine na wakafanikiwa. Ni somo la saikolojia zaidi kwani watanzania wengi walisha kata tamaa na hali ya maisha yao na kwa kiasi kikubwa walikosa kujiamini. Katika kipindi cha miaka minne ya serikali ya Magufuli kumekuwa na mwamko mkubwa kwa watanzania kuamini kuwa wanaweza.Magufuli ni mtu mwenye magic mind yaani ni kiongozi mwenye uono wa ajabu ila mtu wa kawaida au mtanzania mwenye elemu ya kawaida ni vigumu kuweza kujua kipaji cha ajabu ndani ya akili ya Magufuli katika masuala ya uongozi. Nitatoa mfano mmoja tu kwa wenye ufahamu wao wataelewa nini naongea.Suala la Ununuzi wa ndege mpya.Kama kuna kitu kikubwa kakifanya Magufuli katika uongozi wa nchi katika kipindi cha miaka minne basi ni Ununuzi wa ndege. Watanzania wengi walikuwa wakiona ndege ni big deal kitu ambacho kipo nje yq ya uwezo wao ni kitu cha anasa na isingewezekana kwa sasa kwa watanzania kuishi kwa maisha ya ndege ni maisha ya watu wa ulaya tu. Kwa hivyo ununuzi wa ndege si tu ilikuwa lengo lake kuimarisha usafiri wa anga na kulifufua shirika la ndege Tanzania na kuimarisha utalii bali manufaa makubwa ya Ununuzi wa ndege hizo mpya pengine kuliko yote ni ile hali ya kuwajenga watanzania kisaikolojia kuwa wanaweza na hakuna linaloshindikana katika kutafuta maendeleo na bahati njema mwitiko umekuwa mkubwa mno kwa watanzania kushiriki kwenye kuijenga Tanzania mpya kiakili,kifikra na kwa vitendo. Ila tukiri katika kipindi cha miaka minne cha uongozi wa Magufuli tujiulize nini kikubwa cha maana hasa kilichokamiliswha katika sekta ya michezo? Binafsi kwa upande nathubutu kusema hakuna. Na ni moja ya sekta inayochechemea sana. Inagawaje kumekuwa na mwanga kidogo kama kwa timu ya taifa kufuzu Afcon na Simba kuleta msisimko zaidi klabu bingwa Africa na kufika robo fainali, ila bado kazi sana inahitajika kufanywa kwenye sekta ya michezo ili Tanzania tuwe washindani wa kweli kunako michezo. La kushangaza ni kwamba watanzania tuna mazingira mazuri ya kutuwezesha kufanya vyema kwenye mchezo ila inaonesha mazingira ya akili zetu bado kuna vumbi na tunakiwa kuzisafisha ziadi ili zifanye kazi vyema zaidi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic