April 30, 2019

BEKI Kisiki wa timu ya Tanzania Prison, Salum Kimenya amesema kuwa mkakati wao ni kuona wanashinda mchezo wao unaofuata dhidi ya Yanga utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Mei 2.

Kimenya amekuwa akitimiza majukumu yake ndani ya kikosi cha Prisons ambapo mpaka sasa kwa upande wa mabeki yeye ni namba moja kwa kutupia nyavuni akiwa amefanya hivyo mara saba.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kimenya amesema kuwa tayari kikosi chao kimetia kambi Dar kwa ajili ya kuzoea mazingira na kujiandaa na mchezo wao muhimu kwao.

"Tumejipanga na tupo hapa kwa muda mrefu kujiandaa kuikabili Yanga, nina imani kwa maandalizi ambayo tunayoyafanya tutapata matokeo na hatuna mashaka yoyote.

"Ushindani kwa sasa ni mkubwa nasi tunapambana ili kuona msimu ujao tunaoendelea kubaki kwenye ligi hizo ndizo hesabu zetu kwa sasa mashabiki watupe sapoti," amesema Kimenya.

Yanga wanakumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Sokoine, walipoteza kwa kufungwa mabao 3-1.

2 COMMENTS:

  1. Mwandishi kuwa makini na unachoandika yanga haikufungwa na prison katika hiyo mechi

    ReplyDelete
  2. Yanga won 3-1 hiyo mechi. Hii source unatumia achana nayo...ni tomato sauce!😂

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic