August 31, 2020

 


KIKOSI cha Simba, leo Agosti 31 kimeibuka na ushindi wa mabao 6-0 mbele ya AFC kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha. 


Mabao ya Simba yalifungwa na Meddie Kagere dakika ya nne kwa pasi ya Ibrahim Ajibu ndani ya 18, bao la pili lilifungwa na Larry Bwalya dakika ya 24 kwa pasi ya Ajibu na bao la tatu lilifungwa na Kagere dakika ya 34 kwa pasi ya Gadiel Michael. 


Mpaka muda wa mapumziko Simba ilikuwa mbele kwa mabao 3-0 huku AFC ikiwa haijaambulia bao ndani ya dakika 45.


Kipindi cha pili Simba ilipachika mabao mengine matatu kupitia kwa kiungo wao Luis Miqussone aliyefunga 'hat trick' ambapo alifunga bao la nne dakika ya 64  kwa shuti la nje ya 18 baada ya kipa wa AFC kutema mpira.


Bao la tano lilipachikwa dakika ya 76 kwa pasi ya Said Ndemla na kuzamisha bao kambani na bao la sita lilipachikwa dakika ya 88 baada ya mabeki wa AFC kujichanganya namna ya kukaba.


Simba wanajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu unaotarajiwa kuchezwa Septemba 6 Uwanja wa Sokoine na AFC wao wanajiandaa na Ligi Daraja la Kwanza.

9 COMMENTS:

  1. Waliyoitwa majina ya aibu na kocha wao, wameshindwa mpira wamehamia kudhalilisha wenzao kisa kavaa jezi isiyoendana na timu yao! Ustaarabu kazi kwelikweli bora waendelee tu kubweka.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Eeh kwani ili ni tukio la kwanza kwenye utani wa jadi? simba wamekuwa wakifanya Yanga wamefanya. mnachotafuta ni kufanya kutia doa siku ya mwananchi kwa kuwa mnajua ilifana kuliko siku ya mikia. yaani mnashangaza sana.

      Delete
  2. Hivi mbona siku ya simba day Kuna mmoja shabiki kindakindaki ya Yanga alikuwa anaangalia mpira na mashabiki WA simba na hakufanywa kitu?hawa mbumbu fc wanapaswa kubadilika mpira umewashinda wanabaki na hasira

    ReplyDelete
  3. Hapo Mnyama ameanza unyama wake kwa hodi ya G6. Mumpishe mumpe njia au atawalaza chali na Morris wakimuona hivi hivi bado wakiendelea kumsifu kwa bao lake dhidi ya myama kuzidi kunyanyua morali yake Bila ya kujijuwa wenyewe

    ReplyDelete
  4. Huwezi kutegemea ubinadamu kwenye watu wenye rabia za kinyama. Kumdhalilisha shabiki wa Simba aliyekuha kuangalia mpira na sherehe ni ukatili na ujinga usio na nafasi kwenye jamii ya mpira.
    Ingekuwa ni mashabiki wa Simba ndio wamefanya tukio hilo zingeandikwa makala kem kem kukemea ujinga huo.
    Makanjanja pamoja na kupenda timu yenu simamieni ukweli.

    ReplyDelete
  5. Nyinyi washabiki wa simba mi naona mnapata tabu na hawa watu wanajifanya wana furaha lakini moyoni wana majonzi, we ushasahu mechi zetu za ligi ya mabingwa walikuwa wanakuja wanawashangilia wageni na simba tulikuwa tunaawangalia tu lakini kwenye mechi yao ya Zesco kuna washabiki wa simba walipigwa, sasa hawa watu wanafikiri simba hawawezi kufanya vurugu siku washabiki wa simba wakiamua utasikia TFF ni simba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mlishawahi kung'oa viti. Kwani Kung'oa viti na kumvua mtu jezi nani aliyefanya fujo?

      Delete
  6. Hilo baba Gongowazi limevimba kama Samaki bunju hata halioni aibu linamchania shati huyo kijana mpole alietulia mwenye heshima zake. Baadhi ya Gongowazi hawajui timu mbili hizo ni watani wa jadi ni wajibu Kaka zao wawafahamishe

    ReplyDelete
  7. Hivi ninyi Simba Timu yenu iliundwa/au kuanzishwa ukanda wa Gaza?mna viapo na laana za mitaa ile why?kwani vurugu za Simba na Yanga zimeanza leo? Ustarabu wa Hans Pope kuwa Kamati ya usajili Simba akamsajili Morrison ,halafu yupo Kamati ya hadhi za Wachezaji na akakaa Kama mtoa hukumu na mkashinda kwa wingi wenu ,kwa hilo tukio tu utauliza nani mstaarabu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic