April 7, 2019


Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Yanga, mgombea ambaye alijitokeza katika uchaguzi wa awali, Yono Kevela, amefunguka kuwa bado yupo njia panda kama arudi kugombea nafasi aliyoitaka au aendelee na mambo mengine.

Katika uchaguzi wa awali ambao ulitarajiwa kufanyika Januari 13, mwaka huu, Kevela alijitokeza kugombea nafasi ya makamu mwenyekiti wa klabu hiyo na uchaguzi huo, ulikuwa kwa ajili ya kujaza nafasi ambazo ziko wazi ikiwemo ile ya mwenyekiti iliyoachwa na Yusuf Manji.

Yanga imebadili utaratibu wake ambapo uchaguzi wa safari hii utafanyika kwa jumla tofauti na ule wa awali ambao ulikuwa wa kujaza nafasi zilizo wazi na unatarajiwa kufanyika Mei, mwaka huu. Akizungumza na Championi Ijumaa, Kevela alisema:

“Bado sijatoa maamuzi kama niendelee na hili la kugombea uongozi hapa Yanga au nifanye mambo mengine, hilo ndiyo nimekuwa nikijiuliza sana kutokana na jinsi mambo yanavyokwenda.

“Sisi ambao tuligombea awali tuliambiwa kuwa safari hii tutachukua fomu tu na kufuata taratibu nyingine sababu awali tulikuwa tumelipia, hivyo mimi naweza kusamehe hata hizo fedha kama sitaendelea kugombea uongozi sababu bado kuna mambo hayajawa sawa.”

Ikumbukwe uchaguzi wa Yanga, awali ulivurugika kutokana na baadhi ya wanachama kutoka mikoa mbalimbali kwenda mahakamani kupinga uchaguzi huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic