April 2, 2019


Imeelezwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga Mzee Ibrahim Akilimali amendelea kusisitiza Baraza la wadhamini hawana mamlaka ya kuteua uongozi wa muda ndani ya klabu.

Akilimali amefunguka kwa kueleza kuwa watu pekee wenye mamlaka ya kufanya uteuzi wa viongozi wa muda ni sekretarieti ya klabu pekee.

Ameeleza kuwa hawautambui uongozi wa muda uliotangazwa na Baraza la Wadhamini Yanga kwa wao kama Baraza la Wazee.

Ikumbukwe siku chache zilizopita, Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini, George Mkuchika, alitangaza wajumbe wa muda wa Kamati ya Utendaji Yanga jambo ambalo Akilimali amepingana nalo vikali.

Tayari wajumbe hao wameshaanza kufanya kazi ikiwa ni kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Mei 5, 2019.



7 COMMENTS:

  1. Huu utaratibu wa kumpa Akilimali airtime kwny blog yako inakutoa credibility co kila habar una ruka nayo watch it not to that extent bro

    ReplyDelete
  2. Mimi nadhani nyinyi wanachama na wapenzi wa Yanga punguzeni munkari na jazba kuna mambo muhimu wa hiyo kamati kuyashughulikia acheni kuwatia midomoni wakiamua kuikana hiyo kamati mambo yatakuwa magumu zaidi lazima mfikirie hapo hiyo mnayoiita sekrtarieti imeshindwa haina ubavu wa kuisaida timu kaeni mfikiri hapo kwanza.

    ReplyDelete
  3. Hivi na nyie waandishi hamna watu wa kuwafanya interview? Yaani muda mwingine tunajisikkia kichefuchefu kutuletea habari za akilimali.

    ReplyDelete
  4. Kwani hilo Baraza la wazee lipo kikatiba na Kama halipo huyu babu anafanya nini yanga kuna wakati akiwashambulia wapinzani wa yanga anaungwa mkono lakini akiikosoa yanga anaitwa majina mabaya tink brothers

    ReplyDelete
  5. Hichi kinachofanya na Blog yako si sawa na ni chanzo kikubwa cha kuchochea migogoro kwenye Klabu ya Yanga Watanzania ni waelewa sio mbumbu kamati iliyoteuliwa ilielezwa kinaga ubaga sio interim commitee ni kamati ya kusimamia team only, wewe ndiokwa Elimu yako kweli umeshindwa kumuelewesha huyo Mzee na unajaribu kupandikiza sumu hili Yanga ifurugane wewe Blog yako iendelee kupiga pesa acha hayo mambo kwa maslahi yako angalia na maslahi mapana ya klabu ya Yanga

    ReplyDelete
  6. Mimi nafikiri huyu Mzee ajielewi Kwan nini maana baraza la wadhamini, baraza la wadhamini ndiyo wanaomiliki klabu kwa niaba ya wanachama sasa Kama wao ndiyo. Wamiliki wa klabu na klabu ni pamoja na uongozi, wachezaji na Mali zote zinazomilikiwa klabu sasa ndiyo hivyo wanakuwaje Hawana mamlaka ya kuteua viongozi wa mpito WA Kalinda Mali zao Ikisuburi utaratibu kufuatwa na hiyo secretariet anayosema Iko wapi wakati viongozi wote wamejiuzulu nafikiri huyu Mzee anatumika vibaya

    ReplyDelete
  7. Kama uliwahi kisikoa Rwanda baadhi ya vyombo vya habari vilichangia mauaji ya Kimbari, mfano wake Ni kama huu. Mzee huyu ni mvugaji tu wkt mwingine aachwe.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic