April 10, 2019

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kuna ugumu kwa kikosi chake kutwaa ubingwa kwa sasa kutokana na viporo walivyonavyo Simba.

Yanga wamecheza michezo 30 mpaka sasa wakiwa na pointi 71 nafasi ya kwanza kwenye msimamo, wamebakiwa na michezo nane tu kukamilisha mechi zao 38 kwenye ligi msimu huu, huku Simba wakiwa wamecheza mechi 22 wakiwa na pointi 57 nafasi ya tatu.

Zahera amesema kuwa ni mechi nyingi kwa Simba na anahofia kama Simba atashinda mechi zake zote hatakuwa na nafasi ya kubeba ubingwa kama ambavyo amekuwa amepanga.

"Hizi mechi kumi na sita ni nyingi sana kwa Simba, ni sawa na nusu michezo ya Ligi Kuu Bara ambayo timu inatakiwa icheze, mimi sikuona sababu timu inakuwa na viporo vingi.

"Hili linaweza kuleta matatizo kwani ikitokea timu ikashinda mechi zake zote itakuwa ni rahisi kwao kutwaa ubingwa," amesema Zahera.

3 COMMENTS:

  1. huyu jamaa anatumiaga nini kufikiria?sasa urahisi hapo upo wapi?mbona yeye hakushinda mechi zake zote alizocheza?akili ndogo sana hizi ndio madhara ya makocha wa bure matokeo yake unaparamia watu walioshambuliwa na ebora kichwani

    ReplyDelete
  2. Bro wewe ndie mwenye akili ndogo na hujui mpira na mbinu zake !! ndio maana utaona mechi za kimataifa zinachezwa siku na kwa wakati ule ule ili kutotoa fursa ya kupanga mechi na hili ndilo analozungumzia Zahera

    ReplyDelete
  3. Nashauri bodi ya ligi na TFF wasimamishe ligi hadi siba atakapofikisha idadi ya mechi 30 then ligi iendelee kwa timu zote zingine.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic