April 7, 2019


LIGI ya Soka la Ufukweni inayoendelea kwa sasa kwenye uwanja maalumu uliopo Karume yalipo makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imezidi kunoga huku mashabiki wakiombwa kujitokeza kwa wingi.

Akizungumza na Saleh Jembe, katibu wa mashindano hayo, Abdlah Mitelo amesema ushindani uliopo kwenye ligi ni mkubwa na kuwaomba mashabiki wajitokeze.

"Mashindano yanazidi kupamba moto na ushindani unaonekana, ombi langu kwa mashabiki kujitokeza kuona namna ligi inavyokwenda pamoja na kufaidi soka safi la vijana, nina amini wakijitokeza kwa wingi itasaidia kuukuza mpira wetu kwani hakuna kiingilio," amesema Mitelo.

Matokeo ya mechi za leo kwenye ligi hiyo ambayo kwa sasa ipo mzunguko wa tano ni kama ifuatavyo:- Vingunguti Kwanza imeshinda mabao 6-2 dhidi ya Buza FC, Tanzania Prisons imeshinda mabao 8-4 dhidi ya Mburahati FC na Friends Of Mkwajuni imeshinda mabao 6-5 dhidi ya Ilala FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic