April 23, 2019


Madrid kumuuza Bale

Real Madrid wanaangalia uwezekano wa kumuuza mshambuliaji wao Gareth Bale kutoka Wales msimu ujao au wamtoe kwa mkopo ikiwa hawatapata mteja mzuri. (Marca)

Bale anaweza kujiunga na Manchester United kwa mkataba wa deni ambapo anaweza kulipwa £5m. (Marca, via Mirror)

City kuvunja benki ili kumsajili Rodri

Manchester City wako tayari kuvunja rekodi ya uhamisho ya £60m ili kumsaini mkataba na Rodri ambaye yuko katika fomu nzuri hici sasa. 

Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Spain anayekipiga Atletico Madrid anayeweza kujaza nafasi ya Mbrazili Fernandinho, mwenye umri wa miaka 33. (Telegraph)

Tottenham yafyngua milango kwa Trippier

Tottenham wamejiandaa kumuuza mchezaji Kieran Trippier msimu ujao huku Manchester United na Napoli wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Sun)

Emery kuongeza mkataba Arsenal

Unai Emery aliyechukua nafasi ya Arsenal Wenger anatajwa kuasaini mkataba mwingine na Arsenal msimu huu . (mail)

Barcelona kumtoa kwa mkopo Vidal

Barcelona wanatarajia kumtoa mchezaji wao wa kimataifa kutoka Chile Arturo Vidal. (Sport)

Man United yatoa ombi kwa Bayern Munich.

Manchester United wametoa ombi la  euro milioni 60 (£51.9m) kwa Bayern Munich wakiomba wasaini mkataba na Niklas Sule mwenye miaka 23 kwa msimu unaokuja . (Sport 1, via Teamtalk)

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic