April 23, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameweka wazi kuwa nia yao ni kuwafunga wapinzani wao Azam FC kwa ajili ya kuongeza gepu la pointi lakini pia kujiwekea mazingira mazuri zaidi ya kuelekea kutwaa ubingwa.

Yanga watapambana na Azam FC kwa mara ya kwanza msimu huu katika mechi itakayopigwa Jumatatu ijayo Uwanja wa Taifa, Dar. Mechi hiyo itakuwa ya ushindani mkubwa kutokana na timu hizo kufukuzana kwenye msimamo.

Zahera amesema anajua mechi hiyo itakuwa ngumu na ya nguvu kwa pande zote mbili kutokana na kuhitaji matokeo ambayo yatawafanya kila mmoja kujiweka katika mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi.

“Najua wazi mechi yetu na Azam FC itakuwa ngumu na ya nguvu kwetu kwa sababu sisi wote tunataka tushinde mechi hiyo ili tuzidi kujiwekea mazingira mazuri katika ligi.

“Tunajiandaa tushinde ili tuwaache mbali wapinzani wetu, hii ni mechi ambayo tunahitaji matokeo zaidi na tutapambana kwa ajili ya hilo,” alisema Zahera.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic