April 19, 2019


MENEJA wa timu ya Manchester United, Ole Gunnar Solkskjaer, amesema kuwa kwa sasa hana presha na mechi zake tatu zinazofuata za Ligi Kuu England kwani anaimani na kikosi chake hakitamuangusha.

Manchester United walitolewa na Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa jumla ya mabao 4-0 sasa wameelekeza nguvu zao kwenye mechi za Ligi Kuu England.

"Sina mashaka na mechi zinazofuata kwenye ligi kuu kwa sasa nina imani na kikosi changu tupo tayari kupambana hasa kwa mechi zetu tatu zinazofuata," amesema.

Mechi tatu zinazofuata kwa Manchester United ni pamoja na ule dhidi ya Everton utakaopigwa Aprili 21 Jumapili, Manchester City itakuwa ni Jumatano ya Aprili 24 na wa mwisho kati ya hiyo mitatu anayoipigia hesabu ni dhidi ya Chelsea Jumapili , Aprili 28.

1 COMMENTS:

  1. Many kazeni mechi yenu na mancity ili muingie top four na pia mtubebe sisi ........ Kuchukua kilaini ubingwa epl

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic