MAXIME: MIMI NDIYE KIBOKO YA SIMBA
BAADA ya Kagera Sugar juzi Jumamosi kuifunga Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, kocha mkuu wa timu hiyo, Mecky Maxime amesema kuwa yeye ndiye kibako ya Simba.
Maxime amefikia hatua hiyo baada ya kufanikiwa kuiongoza Kagera Sugar kujiandikia rekodi ya kuwa mwiba mkali kwa Simba kila inapokutana nayo kwenye Uwanja wa Kaitaba mijini Bukoba.
Tangu ajiunge na timu hiyo, msimu wa 2016/17 akitokea Mtibwa Sugar, amefanikiwa kuiongoza timu hiyo kushinda mechi tatu dhidi Simba kati ya sita ambazo imecheza nyumbani na ugenini.
Katika mechi hizo, mbili imeshinda kwenye Uwanja wa Kaitaba huku moja ikishinda kwenye Uwanja wa Taifa ambao ni uwanja wa nyumbani wa Simba.
Maxime amesema kuwa ukiachana na rekodi hizo lakini pia hata wakati alipokuwa Mtibwa Sugar, Simba ilikuwa haimsumbui.
“Siku zote nimekuwa nikisema kuwa makocha ambao tunaweza kuizuia Simba isipate ushindi ni mimi, kwani nimekuwa nikifanya hivyo mara nyingi tu.
“Hii ni kutokana na kuijua vizuri timu hiyo lakini pia mbinu ambazo imekuwa ikizitumia kupata ushindi, kuna wachezaji katika kikosi cha Simba cha sasa ukiwadhibiti vilivyo basi unakuwa umemaliza kazi,” alisema Maxime.
CHANZO: CHAMPIONI
Sasa kwanini asisubiri asifiwe na kama yeye kweli kiboko ya Simba basi aiwezeshe timu yake kubeba ubingwa wa ligi badala ya Simba. Kukamia mechi moja halafu timu inapotea kuna kazi faida gani?
ReplyDeleteHongera kwa kuiweza SIMBA huku ukiishindwa YANGA na the rest of TPL Teams
ReplyDelete