RONALDO AWEKA REKODI YA DUNIA
SHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo, juzi, aliweka rekodi ya pekee baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Italia (Serie A), na timu yake ya Juventus.
Ronaldo anaweka rekodi ya kuwa mchezaji cwa kwanza kihistoria kushinda ubingwa wa Serie A, Premier (England) na La Liga (Hispania).
Juzi Ronaldo alitwaa ubingwa huo baada ya timu yake kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fiorentina.
“Nipo hapa na naamini kuwa nitaendelea kuwa hapa, naamini kuwa msimu ujao nitakuwa hapa kwa asilimia 1000, hapa ni sehemu muhimu kwangu na nimepata mafanikio makubwa sana hapa,” alisema Ronaldo baada ya mchezo huo.
Huu ni ubingwa wa nane mfululizo kwa Juventus kwenye Serie A na ukiwa ni wa 35 kwa jumla.
0 COMMENTS:
Post a Comment