April 12, 2019


MSHAMBULIAJI wa timu ya Mbao FC, Said Junior amesema kuwa kwa sasa kikosi chao kinajipanga kupata matokeo chanya mbele ya Ndanda FC.

Mbao ipo chini ya kocha Salum Mayanga ambaye amepata pointi moja tu kwenye michezo mitatu ambayo amesimamia mpaka sasa.

Junior amesema kuwa wamejipanga kiasi cha kutosha na wana imani mchezo wao unaofuata watapata matokeo chanya.

"Ushindani ni mkubwa kwenye ligi na kila timu inahitaji matokeo, ila ni wakati wetu kupata matokeo kwani muda tunao na uwezo tunao hivyo mashabiki watupe sapoti," amesema Junior.

Mbao itamenyana na Ndanda FC Mei nne Uwanja wa CCM Kirumba ipo nafasi ya 16 baada ya kucheza michezo 33 na ina pointi 37

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic