April 20, 2019


Mjumbe wa Baraza la Wazee Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali amesema kuwa amefurahishwa na mchakato wa uchaguzi wa klabu yake.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya mchakato wa kuelekea uchaguzi kwenda vizuri jambo ambalo limempa furaha juu ya jitihada zilizofanywa na Shirikisho la Soka nchini (TFF).

Akilimali ameeleza kuwa baada ya uchaguzi kukamilika atachinja mbuzi kwa ajili ya kujipongeza.

Mzee huyo amefunguka kuwa Yanga imekuwa haina viongozi kwa muda mrefu lakini sasa amesema mambo ni matamu na anasubiria uchaguzi kwa hamu.

Ameeleza kuwa wameteseka kwa muda bila kuwa na viongozi na sasa tayari wameshapata mwangaza ambao utakamilika rasmi Mei 5 mwaka huu.

Yanga inaenda kufanya uchaguzi mkuu tareje tajwa juu huku ukisimamiwa na TFF kwa maagizo ya serikali kupitia Baraza la Michezo Tanzania (BMT).


1 COMMENTS:

  1. Ukiona hivyo ujue keshakula fungu la mtu halafu anasubir kulianzisha jingine tena.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic