April 20, 2019



KOCHA wa timu ya Serengeti Boys, Oscar Mirambo amesema kuwa leo watapambana kufa na kupona ili kufuta makosa yote waliyoyafanya kwenye mechi mbili za nyuma kwenye michuano ya Afcon.
Serengeti Boys walifungua dirisha la michuano ya Afcon ya vijana chini ya miaka 17 vibaya kwa kupokea kichapo cha mabao 5-4 dhidi ya Nigeria na wakakubali kupokea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Uganda.
Mirambo amesema kuwa wanatambua umuhimu wa michuano hii na uhitaji wa kufuzu kushiriki michuano hivyo leo watapambana kufa na kupona.
"Bado tuna nafasi licha ya kupoteza michezo yetu iliyopita, kwa namna kundi lilivyo bado tuna nafasi ya kufuzu endapo tutashinda na nina amini hilo linawezekana. 
"Morali ya wachezaji ni kubwa na mbinu mpya ambazo tumewapa wachezaji zitasaidia kupata matokeo chanya, mashabiki wajitokeze kwa wingi," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic