AZAM FC leo watakuwa uwanja wa Sokoine wakimenyana na timu ya Mbeya City mchezo wa ligi kuu huku wakisumbuliwa na mzuka wa bao la penalti walilofungwa mchezo wao wa mwisho uwanja huo dhidi ya Tanzania Prisons.
Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ajili ya kupambana leo ila bado wana kumbukumbu za kupoteza mchezo wao wa mwisho.
"Ligi ni ngumu na kila timu inatafuta ushindi hivyo nina amini haitakuwa kazi rahisi, kwani tunakumbukumbu ya kupoteza mchezo wetu uliopita dhidi ya Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Sokoine.
"Wachezaji wana morali kubwa na wapo tayari kupambana ni suala la kusubiri muda tu, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti," amesema Maganga.
Azam FC wamecheza michezo 30 wapo nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kujiwekea kibindoni pointi 63.
0 COMMENTS:
Post a Comment