KOCHA Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kuwa kuelekea kwenye mchezo wake wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Jumatano Uwanja wa Jamhuri, Morogoro atawakosa wachezaji wake wawili wa kikosi cha kwanza.
Zahera amesema kuwa amekuwa akiwapa mbinu wachezaji wake kuelekea mchezo huo wa ligi ambao anaamini utakuwa mgumu.
"Nitamkosa Kelvin Yondani, ambaye alionyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar pia nitamkosa Feisal Salum ambaye ana kadi tatu za njano hivyo hawatakuwa sehemu ya kikosi changu dhidi ya Mtibwa.
"Licha ya kukosekana kwao bado nina upana wa kikosi kwani tayari nahodha wao Ibrahim Ajibu amekuwa fiti kiafya pamoja na beki Abdalah Shaibu 'Ninja' hawa nitawatumia kwenye kikosi changu," amesema Zahera.
Mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Taifa, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Mtibwa Sugar.
Kocha usizoee kuwapa mapumziko zaidi ya siku 2 wachezaji wakibongo kasi yao na utimamu wa kimwili na utayari wa mashindano unashuka....timu inatakiwa iwe kambini na uifuatilie kwa ukaribu na uongeze ufundishaji, nguvu, stamina na mbinu....wachezaji wa Yanga wanachoka haraka
ReplyDelete