April 23, 2019


WAKALA wa mchezaji wa Simba, Mnyarwanda, Meddie Kagere ambaye ni Patrick Gakumba, amefunguka na kusema mazungumzo kati yake na mabosi wa Yanga yanakwenda vizuri na kinachosubiriwa ni kukubali masharti aliyoipa timu hiyo kabla ya kusaini mkataba.

Hiyo, ikiwa ni siku chache tangu ziwepo tetesi za usajili wa mshambuliaji huyo kuwaniwa na Yanga katika usajili wa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara ambao timu hiyo imeandaa bajeti ya shilingi bilioni 1.5 za usajili.

Tuyisenge ni kati ya wachezaji wawili wanaotajwa kutua kusaini kuichezea Yanga akiwemo beki wa kati mahiri wa timu ya taifa ya Congo na Klabu ya AS Vita ya DR Congo, Yannick Bangala Litombo.

Gakumba alisema juzi aliwasiliana na viongozi wa Yanga kwa njia ya simu na kuwapa masharti mawili, kati ya hayo wamhakikishie mshahara wa kila mwezi kabla ya kusaini mkataba wa kuichezea timu hiyo.

Gakumba alitaja sharti lingine ni kukubali dau la fedha ambalo mchezaji wake atalitaka, hivyo kama masharti hayo watayatimiza, basi atatua kukipiga Jangwani katika msimu ujao.

Aliongeza kuwa, ametoa sharti hilo la mshahara kwa hofu ya mchezaji wake kutaabika baadaye baada ya kusaini Yanga na kikubwa hataki kuona mchezaji wake akipata matatizo hayo.

“Juzi niliongea na viongozi wa Yanga wakionyesha nia kubwa ya kutaka kumsajili Tuyisenge baada ya kuvutiwa naye, hivyo mazungumzo hayo yalikwenda vizuri lakini nimewapa masharti mawili ambayo wanatakiwa kuyatekeleza kabla ya kusaini mkataba.

“Moja, ni kumhakikishia mshahara wa kila mwezi baada ya kusaini mkataba huo na lingine wakubali kutoa dau ambalo mchezaji wangu atalitaka, hivyo kama hayo yote wakiyatekeleza, basi Tuyisenge anakuja Yanga.

“Nashukuru viongozi hao wamenihakikishia kuyatimiza hayo na kuniahidi kuwa hivi karibuni wanatarajiwa kupata mdhamini wa timu hiyo, hivyo nisiwe na hofu,” alisema Gakumba.

Hata hivyo, Gakumba aligoma kutaja dau la usajili wala mshahara wanaotaka kwa kuhofia kuharibu dili, akisisitiza ni mpaka watakapokutana uso kwa uso na viongozi wa Yanga.

2 COMMENTS:

  1. Ni kibiashara zaidi kuitumia Yanga lakini lengo ni kuivutia Simba kuharakisha kumnunua mchezaji huyo na dau kubwa Zaidi. Kila mtu anajua kuwa Yanga hawezi akamechi au kuchukua mchezaji Simba anaemtaka licha ya kuelezwa kuwa bakuli lao linafanya vizuri. Mbinu ya kuitumia Simba au Yanga kwa mawakala au wachezaji ili kuzishawishi timu hizi kumnunua mchezaji ni jambo la kawaida. Simba na Yanga ni vyema kusajili wachezaji kwa mahitaji ya timu na sio mahitaji ya wakala au mchezaji. Ni vizuri kuangalia uwezo wa Wachezaji wa ndani kwanza na kuwapa nafasi kama wataifakiana nao. Na Kama wataamua kusajili wachezaji wa nje basi basi lazima wawe na ubora wa kweli na maslahi kwa timu. Kwa upande wa kimataifa viongozi wa Simba labda washindwe wenyewe kuifanya timu hiyo kurudi kwa kishindo kimataifa kwani mapungufu ya Simba katika klabu bingwa Africa yalikuwa ya wazi pengine hata kabla simba haijatia mguu katika mashindano hayo. Simba ilikosa uti wa mgongo wa timu wa kweli uliokamilika uwanjani.Nikisema uti wa mgongo ninamaana ya wale wachezaji wanaoijenga timu eneo la katikati ya uwanja yaani mabeki wa kati imara,viungo wa kati imara, washambuliaji wa kati imara na makini. Tunatarajia viongozi wa Simba kwa kutumia uzoefu walioupata klabu bingwa Africa kuijenga Simba imara zaidi na kupiga hatua moja kubwa zaidi Africa mwakani.

    ReplyDelete
  2. mm binafsi najua hawa mawakala wanajua Tanzania n sehemu ya kupga pesa Yanga achaneni na watu wa gharama kubwa mfano kama pesa ipo na mishahara itakuepo Beno aeudishwe suala LA kipa liishe pia wasajili watyu wasiozid watatu na hao hao waliokuwepo wakilipwa tyu kazi inapgika. Et kwa mfano mm napga kazi kila nikiangalia magazeti kuna mtu wa gharama anatafutwa wakati mm silipwi si morale ya kazi inapungua

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic