April 16, 2019

KESHO Simba itakuwa kibaruani kumenyana na Coastal Union mchezo wa ligi kuu Uwanja wa Mkwakwani huku ikitarajiwa kuwakosa nyota wake wawili ambao wanasumbuliwa na majeruhi.

Kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa wachezaji wake wawili bado wanasumbuliwa na majeruhi hivyo bado anasubiri kuona ni namna gani watarejea kwenye ubora wao kuendelea kupambana.

"Pascal Wawa na Juuko Murshid wanasumbuliwa na majeruhi ambayo waliyapata kwenye michezo yetu ya kimataifa hivyo tunasubiri kuona ni namna gani wanaweza kurejea kwenye ubora wao ili waendelee kutimiza majukumu yao.

"Nina kikosi kipana na wachezaji wengi nina amini watatimiza majukumu yao ipasavyo kwani hesabu zetu kwa sasa ni kuona tunapata matokeo chanya kwenye mechi zetu za ligi," amesema Aussems.

Wawa alipata majeruhi kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali dhidi ya TP Mazembe uwanja wa Taifa, na Murshid alipata majeruhi akiwa Congo kwenye mchezo wa pili dhidi ya TP Mazembe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic