BAADA ya Simba kutolewa jana hatua ya robo fainali na TP Mazembe kwa kufungwa mabao 4-1 nahodha msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein amesema kuwa wamenogewa na utamu wa mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo wanajipanga kurejea msimu ujaoa.
Hussein ambaye alionyesha kiwango bora kwenye mchezo wa jana na aliishiwa kuonyeshwa kadi ya njano amesema kuwa bado wana imani ya kuoata nafasi kurejea ligi ya mabingwa msimu ujao.
"Tulianza kwa kuandika kitabu cha Historia mpya ya Soka letu baada ya miaka mingi kupita na tulitegemea kuendelea kukiandika kitabu hicho pale LUBUMBASHI, kabla ya kukifunga lakini haikuwa bahati.
"Uzuri na utamu wa Mashindano haya ya CAF CHAMPIONS LEAGUE unatufanya kama TEAM na Mm binafsi Kupambana Kuhakikisha mwakani tunarudi tena," amesema Tshabalala.
0 COMMENTS:
Post a Comment