UONGOZI wa Azam FC ambayo ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 66 baada ya kucheza michezo 32 umesema kuwa kesho kikosi kitaanza rasmi kupewa mbinu za kuimaliza Yanga kwenye mchezo wao unaofuata wa ligi utakaochezwa Aprili 29 uwanja wa Taifa.
Azam FC iliyo chini ya Idd Cheche huku safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Donald Ngoma na Obrey Chirwa inakutana kwa mara ya kwanza na Yanga msimu huu, huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao uliopita wa ligi dhidi ya Ndanda kwa kufungwa bao 1-0.
Mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema kuwa baada ya mchezo wao dhidi ya Ndanda waliwapa mapumziko wachezaji wao na kesho wataanza mazoezi rasmi.
"Wachezaji wetu wote wamepewa mapumziko baada ya mchezo wetu dhidi ya Ndanda, sasa kesho tunashusha muziki mzima uwanjani kuanza mazoezi kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Yanga.
"Wachezaji wetu wapo vizuri kwa sasa kila mmoja anajua majukumu yake kutokana na uzoefu ambao wanao itasaidia kutupa matokeo chanya," amesema Alando.
0 COMMENTS:
Post a Comment