April 7, 2019


KIKOSI cha Simba jana kililazimisha suluhu ya kutofungana mbele ya TP Mazembe kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa nahodha wa Simba, John Bocco alipaisha mawinguni penalti dakika ya 59 baada ya mchezaji wa TP Mazembe kunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kwa mchezaji kukosa penalti ni kitu cha kawaida hivyo wanaomlaumu wanapaswa watambue mchango wa Bocco ndani ya Simba.

"Atakaemlaumu Bocco kukosa Penati, ni ugeni katika mpira kwa baadhi yetu, Bocco huyu huyu ndio anafunga Penati zote za Simba kila tunapopata, Bocco huyu huyu ndio alifunga Penati muhimu kule kitwe tulipocheza na Nkana.

"Penati ni pigo la bahati na huwa haina mwenyewe, ikiwa Messi mwenye mpira wake hukosa,Captain Bocco ni nani asikose? Ikumbukwe huyu kakosa na Mazembe,kuna mtu juzi tu kakosa na Ndanda.


"Tuwape nguvu wachezaji wetu ili wakapambane kule Lubumbashi,tuache lawama za hovyo hovyo," amesema Manara.


9 COMMENTS:

  1. Achana na penati. Sidhani kama kuna mdau wa soka nchini atamlaumu Boko kukosa penati. Isipokuwa Boko amepoteza hali ya kujiamini katika kufunga magoli kwa muda sasa na licha ya wadau kupendekeza kuongezwa kwa fowadi mwenye uwezo zaidi lakini hakuna kilichofanyika. Wazungu wana msemo wao unaosema if you don't spend enough today you won't satisfy tomorrow.

    ReplyDelete
  2. Watu wake wa simba walalamike yeye kaichomeka na yanga, duh tz bhna

    ReplyDelete
  3. Uyo manara Ana matatizo ya ubongo sio bure,yanga imekujaje Apo,alikuwa anacheza na yanga au Tp mazembe?

    ReplyDelete
  4. Apimwe yule... Sio bure.... Hata anariport nae

    ReplyDelete
  5. Apimwe yule... Sio bure.... Hata anariport nae

    ReplyDelete
  6. Ni kweli boko amepoteza umakini Kwenye upigaji penalti wanasimba lazima tulitambue hilo mapema. Ukiangalia penalti aliyopiga dhidi ya mbao metacha mnata kidogo aitoe penalt ya Bocco. Tubadilishe mpigaji mbona mkude hajawahi kosa na huwa anafunga penalt mhimu za mwisho? Tubadilike mapema kabla haijatuletea shida zaidi.

    ReplyDelete
  7. Waliokuwa wanaitaja Simba kwenye kutembeza bakuli kule Dodoma je? KWANI ni Simba ndio waliokuwa wakichangisha?
    Ingizeni timu kwenye mfuko wa kusaidia familia maskini.
    Kuna mmoja Singida United imemshinda kabaki kusema och nitasajili mmoja
    Tatizo sio kusajili tatizo kulipa mishahara nagharama nyingine za timu.

    ReplyDelete
  8. Bocco bado nichezaji mzuri tu kukosa penat ni kawaida tu mchezaji yeyote anaweza kukosa penat, mashabiki tuache lawama zisizokuwa na mpango wowote

    ReplyDelete
  9. Kukosa penalty au magoli ya bicycle kick kugonga mwamba ni kawaida..Mbona Alahly kapigwa 5 na was kawaida Melody!Simba wamecheza vizuri na takwimu zinaonyesha.mwakani watafika mbali zaidi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic