April 7, 2019


IMEELEZWA kuwa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa Jana Uwanja wa Sokoine kati ya Tanzania Prisons na Biashara United umeingiza kiasi cha shilingi elfu tisa pekee.


Mashabiki watatu tu ndio ambao walikata tiketi za shilingi elfu tatu kwa kila mmoja na kufanya mapato ya siku kuwa shilingi elfu tisa.

Kwenye mchezo wa jana timu zote zilitoshana nguvu na kushuhudia dakika tisini zikikamilika bila kufungana.

Matokeo hayo yanaifanya Prisons kufikisha jumla ya pointi 42 baada ya kucheza michezo 32 ikiwa nafasi ya sita huku Biashara United ikisalia nafasi ya 19 baada ya kucheza michezo 31 ikiwa na pointi 34.

4 COMMENTS:

  1. Ahahahahaaaaaaaaaaaa nmecheka kingoni

    ReplyDelete
  2. Hahahaaaaaaaa wangelifunika goli isipae

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dua za jangwani hizo!waliota 8-0.Hata Alahly alipigwa 5!

      Delete
  3. Duh! Noma sana iyo buku tisa tu, nanyie waandish wa habali msipende sana sifa vipu vingine vyakupotezea tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic