SALEH JEMBE HAIHUSIKI NA TAARIFA ZA MO KULETA SINTOFAHAMU NA KLABU YA SIMBA, PUUZENI
Mtandao wa Saleh Jembe unakanusha taarifa iliyosambaa mitandaoni ikieleza kuwa Uongozi wa klabu ya Simba umeingia kwenye sintofahamu na Mwekezaji wake, Mohammed Dewji 'Mo'.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Blog hii ilizungumza na kiongozi mmoja wa juu wa klabu ya Simba kuwa Mo anataka kumiliki mali zote zote za klabu zitakazoanzishwa chini ya ufadhili wake kwa asilimia 70.
Aidha, taarifa hiyo ilizidi kwenda mbali kwa kueleza kuwa viongozi wa Simba wameshaanza kukaa vikao na wanasheria kwa ajili ya kufanya harakati za kumng'oa mwekezaji huyo haraka ili asifikie maamuzi hayo.
Kwa masikitiko makubwa Saleh Jembe inawaomba radhi wote walioguswa na taarifa hiyo kwa namna moja ama nyingine.
Saleh Jembe haijahusika na uandishi habari hiyo na tunaahidi kuchukua hatua za kisheria kwa aliyehusika kwa kutuchafua.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza na pia kwa uongozi mzima wa klabu ya Simba juu ya taarifa hiyo FAKE ambayo haijaandaliwa na Saleh Jembe.
Ni taarifa ya kuitaka kuitoa Simba mchezoni. Aidha vibaraka wa Mazembe wa hapa nchini ambao wana wivu na maendeleo ya Simba watakuwa wanahusika.Aliepewa kapewa hata mtu afanye majungu ya kiasi gani huwezi mpokonya.
ReplyDeleteHatutaingia katika mtego wa wajinga.
ReplyDeleteJamuna idipokuwa ni walewale wa miaka hote na dena wafahamu kuwa kila ovu litawarejea wenyewe na Simba ikizidi kupaa na wale wakizidi kugaragara
ReplyDeletewatashndw wnyw
ReplyDeletewashindwe mbwa hao
ReplyDeleteHusda nä majungu malipo yake ni kuzidi kuharibikiwa kwa anayeyafanya. Watu wapo uchi hawachutami wanazua nä kufatilia yasiyowahusu.
ReplyDelete