April 16, 2019

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' Oscar Mirambo amesema kesho watapambana mbele ya Uganda kupata matokeo chanya.

Serengeti ilifungua pazia la michuano hiyo kwa kucheza na Nigeria na kupokea kichapo cha mabao 5-4 mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa, kesho itashuka uwanjani kumenyana na Uganda ambayo nayo pia ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Angola na ilifungwa bao 1-0.

Kocha Mirambo amesema vijana wameshafundishwa na kupewa mbinu mpya ukizingatia kwamba wamebakiwa na michezo miwili ili kumaliza mechi za makundi.


 "Tunajua tumeanza vibaya mashindano yetu ila hatujapoteza matumaini tumeyafanyia kazi makosa yetu tunaingia kibabe kupambana na wapinzani wetu Uganda.

"Ushindani upo nasi tumejipanga kuleta ushindani, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona namna tutakavyopeperusha Bendera ya Taifa," amesema Mirambo.


Pia kesho kutakuwa na mchezo kati ya Nigeria na Angola ambao utachezwa pia Uwanja wa Taifa

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic