KAZI IMEANZA!!! KIFAA KIPYA KUTOKA ZIMBAMBWE KUTUA YANGA
Imeelezwa kuwa klabu ya Yanga imeanza harakati za kumsajili mshambuliaji hatari wa klabu ya FC Lupopo ya DR Congo, Roderick Mutuma.
Taarifa imesema kuwa Yanga tayari imetuma maombi ya kumsajili nyota huyo raia wa Zimbabwe mwenye thamani ya dola 113,000 ambazo ni zaidi ya milioni 260 za Kitanzania.
Jeuri ya Yanga kufanya usajili huo inakuja kutokana na harambee ya kuichangia klabu iliyozinduliwa hivi karibuni Dodoma kwa ajili ya kuchanga fedha.
Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera tayari ameshaanza kujinadi kuwa usajili wa msimu ujao utakuwa ni waina yake ili kukiboresha kikosi.
Zahera aliahidi kuwa kwa fedha ambazo zitachangishwa na wanachama pamoja na mashabiki wa timu hiyo zitasaidia katika kununua wachezaji wa maana ndani ya timu.
Usajili wa kwenye magazeti huooo😂😂😂. Time will tell
ReplyDeleteHilo ni porojo la siku zote. Atangojewa mchezaji huyo kama alivokuwa akingojewa Manji
ReplyDeleteNgoja tuone
ReplyDeleteIngonjeeni yanga kwenye ligi ijayo jinsi Zahera atapoleta wachezaji wane anawasifu wanajuwa kifaransa tu. Chapwa
ReplyDelete