April 19, 2019




Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Tanzania, Dkt Harison Mwakyembe ameitaja Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya SportPesa kuwa ni sehemu ya mafanikio ya michezo nchini.

Kauli hiyo aliitoa jana huko Bungeni Mkoani Dodoma wakati akiwasilisha bajeti yake ya michezo kwa Wabunge wa Tanzania.


SportPesa wanatarajiwa kuwaleta nchini mabingwa mara tano wa michuano ya UEFA Europa ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao ya msimu mpya wa 2019/2020.


Akiwasilisha bajeti hiyo, Dkt Mwakyembe alisema katika kufikia mafanikio zaidi, wizara yake itaendelea na mahusiano mazuri waliyoyaanzisha na wadau zikiwemo sekta binafsi katika kukuza na kuendeleza michezo nchini.
Dkt Mwakyembe alisema, SportPesa tofauti na kukuza na michezo nchini imekuwa sehemu ya mafanikio ya miundombinu kwa kuweka nyasi mpya za bandia na kusimamia  utunzaji wake kwa kipindi cha miaka miwili.

    
Aliongeza kuwa, pia SportPesa imefanikisha kuandaa mashindano ya SportPesa Cup ambayo imekuwa ikifanyika hapa nchini kwa mara mbili tangu kuanzishwa kwake 2017.


“Yapo mafanikio mengi ya michezo yamepatikana ndani ya kipindi hichi na hayo yametokana na wizara yake kuwa na mahusiano mazuri mazuri na sekta binafsi na baadhi ya makampuni.


“Kati ya kampuni hizo, ipo SportPesa ambayo imefanikisha kuandaa michuano ya SportPesa tangu mwaka 2017 na Tanzania imefanyika kwa muda wa miaka miwili tangu kuanzishwa kwake.


“Pia, SportPesa imesaidia kuweka miundombinu mizuri hapa nchini mfano ilifanikisha uwekaji wa nyasi bandia mpya kwenye Uwanja wa Taifa, Dar huku ikitumia miaka miwili katika utunzaji wake.


“SportPesa ilifanikisha ziara ya ujio wa klabu ya Everton ya Uingereza hapa nchini na tena juzi imetangaza kuileta klabu ya Sevilla,’ alisema Dkt Mwakyembe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic