April 5, 2019


TP Mazembe rasmi imeingia kwenye rada ya kuwania saini ya kiungo mshambuliaji Mzambia, Clatous Chama na mshambuliaji Mnyarwanda, Meddie Kagere wanaokipiga Simba.

Hiyo, ikiwa ni siku moja tangu Mazembe watue nchini kwa ajili ya kucheza na wapinzani wao Simba katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mazembe ni klabu ya pili kuonyesha nia ya kuwasajili nyota hao ikiwemo AS Vita yaDR Congo inayofundishwa na Florent Ibege ambaye alisema anawahitaji nyota hao kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chake baada ya kuvutiwa na viwango vyao.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, kutoka kwa mmoja wa viongozi waliokuwepo kwenye msafara wa Mazembe, wamevutiwa na viwango vya nyota hao katika michezo kadhaa waliyoitazama kupitia video mbalimbali za mechi zao.

Mtoa taarifa huyo alisema, kwa viwango walivyokuwa navyo wachezaji hao, hawastahili kuendelea kubaki kucheza Tanzania na badala yake kutoka nje kwa lengo la kupata mafanikio zaidi. Aliongeza kuwa, wamepanga kutenga kiasi chochote cha fedha kwa ajili ya kuwang’oa nyota hao wa Simba ili watue Mazembe kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chao katika msimu ujao wa 2019/20.

“Kiukweli kabisa Chama ni bonge la kiungo na lipo wazi tulikuwa tukimfuatilia muda mrefu, ni mchezaji hatari mwenye uwezo wa kufunga na kutengeneza mabao ndani ya wakati.

“Anacheza kwa kutumia akili nyingi akiwa na mpira, ni mchezaji wa kuchungwa kama sisi Mazembe tayari tumechukua tahadhari juu yake na kikubwa ni kutompa nafasi ya kumiliki mpira muda mrefu kwa hofu ya kutudhuru.

“Pia, Kagere yeye anacheza kwa kutumia nguvu nyingi na ana uwezo mkubwa wa kufunga mabao kwa staili yoyote, hivyo kwetu Mazembe tumeona kuwekeza nguvu kwao katika usajili na tupo tayari kutumia kiasi chochote cha fedha kuwasajili nyota hao,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Swedy Mkwabi kuzungumzia hilo alisema: “Hakuna mchezaji yeyote muhimu katika timu tutakayemuachia hivi sasa na badala yake tunaendelea kukiimarisha kikosi chetu zaidi, kama unavyofahamu malengo yetu tumeyaelekeza kimataifa.”

3 COMMENTS:

  1. Hizo taarifa za Mazembe za kuwataka wachezaji wa Simba ni moja ya janja ya Mazembe kuwavuruga akili wachezaji wa Simba kwenye mechi ya jumamosi na hawatafanikiwa. Sijaona wakati ambao wakongo wakiingia mchecheto kwa klabu za Tanzania kama mara hii kwa Simba. Kwa kifupi Mazembe keshakubali kufungwa na Simba ila ni Simba wao wenyewe wachague idadi gani ya magoli wanataka kuifunga Mazembe. Kwa umati wa mkapa Simba wakifanikiwa kupata goli la mapema watawachanganya Mazembe na kuweza kupata magoli mengi zaidi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. KAMA NI UJANJA WA NYANI NA SIMBA WASEME INAWASAINISHA WACHEZAJI 3 WA TP MAZEMBE HUKU TUKIJUA NI MBINU YA KUWAVURUGA NAWAO KAMA WATAAMINI. MBINU HUJIBIWA KWA MBINU.

      Delete
  2. Wanaonesha dharau wanafikiri Simba masikini na sisi vilevile tunawataka wachezaji wao na pesa ipo ya kuwanunua kwa helaimnayouitaka. Tazameni nyota wa timu nyengine ambao yimu zao zipo hoi kifedha na mtapata wachezaji kwa bei cheee tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic