April 5, 2019


Shabiki wa Simba aliyetembea kwa miguu kutoka jijini Mbeya kuja Dar es Salaam, tayari ameshawasili Makao Makuu ya klabu hiyo.

Shabiki huyo ametembea kutoka Mbeya kwa ajili ya kuja kuisapoti timu yake ambayo itacheza kesho dhidi ya TP MAzembe kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba itakuwa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali utakaoanza majira ya saa 10 kamili za jioni.

Imeelezwa kuwa shabiki huyo amekabidhiwa tiketi kwa ajili ya kuushuhudia mchezo wa kesho na imeelezwa anaweza akakutana na mabosi wa klabu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic