SINGIDA United leo imekubali kulazimisha suluhu na KMC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Namfua.
Mchezo huo uliokuwa na ushindani kwa timu zote ambapo zilikuwa zikishambuliana kwa zamu ulishuhudiwa dakika 90 zikikamilka kwa timu zote kutoshana nguvu.
Huu unakuwa mchezo wa kwanza kwa KMC kuambulia pointi ugenini baada ya kupoteza jumla ya pointi tisa hivi karibuni kwa kuanza mbele ya Yanga, Ndanda na kisha nyingine waliziacha pale Sokoine kwa Mbeya City.
Singida United nao pia unakuwa ni mchezo wa kwanza kugawana pointi moja kati ya miwili ya karibuni ambapo walianza mbele ya Alliance kubeba pointi tatu na kumaliza na Kager Sugar uwanja wa Namfua.
Timu zote mbili zilifundishwa na Felix Minziro na ndiye aliyezipandisha timu hizo kushiriki ligi kuu.
0 COMMENTS:
Post a Comment