April 15, 2019


MSHAMBULIAJI wa Yanga Heritier Makambo raia wa DR Congo ameweka rekodi msimu huu kwa kuweza kufikisha mabao 15 katika Ligi Kuu Bara.

Katika msimamo wa wafungaji wa ligi kuu mshambuliaji wa Mwadui, Salum Aiyee anashika namba moja akiwa nayo 16 wakati Makambo akiwa nayo 15 huku straika wa Simba, Meddie Kagere akiwa na mabao 14.

Mara ya mwishomshambuliaji wa Yanga wa mwisho kufikisha idadi ya mabao hayo alikuwa ni Simon Msuva ambaye kwa sasa anacheza soka la kulipwa nchini Morocco katika timu ya Diffa Al Jadida kwa kufunga mabao 14 huo ulikuwa msimu wa 2016/17.

Wakati msimu uliopita aliyekuwa mshambuliaji hatari wa Yanga, Obrey Chirwa hakufikisha idadi hiyo na kuishia kumaliza akiwa na mabao 12 wakati kinara wa mabao Emmanuel Okwi wa Simba, aliyefunga mabao 20.

Hivyo Makambo amebakisha mabao 6 tu kuvunja rekodi iliyowekwa na Amissi Tambwe ya msimu wa 2015/16 ya kufunga mabao 21 katika ligi kuu

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic