Licha ya kufungwa bao 4-1 dhidi ya TP Mazembe katika Ligi ya Mabingwa Barani Afrika juzi, timu ya Simba imeweza kuandika rekodi ya kufunga bao ugenini.
Simba katika mechi zake nne tangu iingia hatua ya makundi ilikuwa haijawahi kufunga bao lolote ugenini kwenye mashindano hayo.
Bao pekee la ugenini ambalo Simba walilipata juzi ilikuwa ni dhidi ya Mazembe na likiwa la mapema zaidi kunako dakika ya pili ya mchezo.
Bao hilo alilofunga Okwi liliweza kuipa Simba rekodi ya aina yake kwenye mashindano haya makubwa Afrika kwa ngazi ya klabu.
Tayari wekundu hao wa Msimbazi hivi sasa wapo nchini na sasa wanajipanga kwa ajili ya mechi zijazo za Ligi Kuu Bara ili kuutetea ubingwa wao.
Hongera Simba walipofikia wanastahiki pongezi. Hongera viongozi wa Simba kwa jitihada zao zilizotukuka kuhakikisha wachezaji wao wanapata karibu kila wanachokihitaji ili kuwarahisishia majukumu yao ya kazi.Hongera sana wachezaji na benchi la ufundi kwa hakika walipambana vya kutosha wanastahiki kila pongezi tena sana.Hongera sana mashabiki wa Simba hakika kama kuna kitu watanzania tunapaswa kujifunza katika kujali vya kwetu basi tusione aibu kuwaiga mashabiki na wanachama wa Simba na TFF watakuwa wachoyo wa fadhila kama isipotambuwa hamasa za mashabiki wa Simba. Vile vile pongezi za pekee zimuendee muekezaji na shabiki nguli wa Simba Moahamedi Dewji kwa kweli ameleta uhai Simba. Kumekuwa na Majungu kadhaa juu ya Mo na jitihada zake za kuhakikisha Simba inakuwa moja ya klabu kubwa na tishio barani Africa. Kutoitakia Simba mafanikio ni kutoitakia nafanikio Tanzania.
ReplyDeleteIngawaje kwa bahati mbaya kuna watanzania ambao hawajifichi kuiombea mabaya nchi yao itakuwaje Simba? Ila Mwalimu Nyerere baba wa Taifa la Tanzania aliwahi kutoa kisa cha wanaume ambao walizamiria kwenda kumuoa binti mmoja mrembo ambae makazi yake yalikuwa mlimani na ili kumfikia na kukamilisha posa yake basi lazima uwe mwanaume wa kweli usietingishika na vitisho na vioja vya maneno ya kipumbavu kwani licha ya ugumu wa kuupanda mlima kumfikia binti mrembo lakini safari yake ilijaa vitisho vya ajabu na moja kati ya mashariti mazito ya safari hiyo ya kwenda kumchumbia binti mrembo wa mlimani kwa mujibu wa simulizi ya baba wa Taifa mwalimu Nyerere ni kwamba mtu hatakiwi kugeuka nyuma hata kama mtu atahisi anapapaswa na sharubu za Simba mgogoni kwani ukigeuka tu basi unageuka jiwe. Na kwa mujibu wa simulizi wengi tu waliojaribu kumfuata huyo mchumba waliishia njiani na kugeuka mawe.Na mawe mengi ya watu yalirundikana zaidi karibu ya kumfikia mchumba huyo kwani ilikuwa kila mtu akimkaribia huyo mchumba ndio vitimbi vilikuwa vikizidi kiasi kwamba ilikuwa sio rahisi mtu kubeza anachokisikia na kuamua kuacha kufokasi na safari ya mafanikio na kuanza kufokasi na maneno ya kukatisha tamaa na kujikuta wakifeli. Maneno ya chokochoko tunayoyasikia juu ya Simba,juu ya Mohamedi Mo ni ishara nzuri yakwamba Simba inafanya vizuri na safari ya Simba kuelekea mafanikio ya kweli haipo mbali tena it is about time. Ni kuwaomba tu viongozi wa Simba na hasa Mo kuongeza Dozi ya safari ya Simba kuelekea mafanikio ya kweli ya simba kwani kwa kipindi kifupi tu chini ya management ya Mo na timu yake,Simba tayari inatisha nje ndani ya uwanja. La msingi ni kuisuka timu zaidi kwa ajili ya mashindano ya Africa msimu ujao. Sio vibaya kusema kuwa kikosi cha Simba kinahitaji kufumuliwa na kusukwa upaya kukizi mahitaji ya Africa.Mfano mmoja tu wa mechi ya Mazembe unatosha,sijui kama viongozi walifanya kwa makusudi au kwa bahati mbaya lakini Simba ilikwepa hujuma zote za Mazembe ,wachezaji waliahidiwa mamilioni ya pesa,timu ilipata maandalizi ya kutosha kabisa lakini tumekwenda kupigwa kama watoto vile. Sasa nini maana halisi ya funzo ya mechi ya kwa mazembe? Ni kwamba wachezaji tulionao hawakuwa wanatosha kisawa sawa kukabiliana na timu ngumu za Africa.Tunaposema Africa ni nje ya Tanzania tuwe na timu angalau ikathubutu kupata matokeo ya sare ugenini zidi ya timu vigogo vya Africa. Ushauri kuelekea usajili wa msimu ujao ili kuifanya Simba kuwa bora zaidi ya msimu huu ni(1)kutumia nafasi kumi za wachezaji wa kigeni kusajili wachezaji wenye viwango hasa na wenye nizamu.(2) kutafuta wachezaji wazawa wenye mapenzi na Simba na wenye nizamu ya kutosha na wenye kujitambua.Na ikiwezekana watafutwe wachezaji wazawa walioshiba kimaumbo ili kumechi na timu za wenzetu amabo wachezaji wao wengi wameshimba kikazi.(3) Simba hakuna haja ya kusubiri mpaka wakati wa mashindano ndio kukutana na timu kubwa Africa ipo haja ya kutafuta mechi nyingi za kujipima nguvu ugenini iwezekanavyo za majaribio ili kuwazowesha wachezji mazingira tofauti na kuwapa uzoefu zaidi.