April 2, 2019


Tetesi za soka barani ulaya leo Jumanne ya Aprili 2, 2019

Herrera asaini mktaba wa awali na PSG

Kiungo wa Manchester United Ander Herrera, 29, amesaini makubaliano ya awali na klabu ya Paris St-Germain ili ajiunge na miamba hiyo ya Ufaransa mwishoni mwa msimu. (Daily Record)

United wazidi kutia ngumu kumuongezea mshahara Herrera

Manchester United wamegoma kumuongezea mshahara Herrera licha ya kujua kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kumpoteza kiungo huyo raia wa Uhispania bure ifikapo mwisho wa msimu. (Telegraph)

Tottenham kuvunja rekodi ya usajili kwa Keane

Tottenham wanaweza kuvunja rekodi yao ya usajili kwa kutoa kitita cha pauni milioni 50 ili kumsajili beki wa Everton na raia wa Uingereza Michael Keane, 26, ambaye amekuwa pia akinyemelewa na Arsenal.(Express)

Costa aanza kuwindwa na Tottenham

Tottenham wamejitosa kwenye mbio za kumsaini mshambuliaji wa Juventus Douglas Costa mwishoni mwa msimu. Mshambuliaji huyo mwenye miaka 28 pia anafuatiliwa na na vilabu vya Manchester United na Manchester City, wakati Chelsea na Paris St-Germain hapo awali walikuwa wakihusishwa na mshambuliaji huyo raia wa Brazil. (Tuttosport, via Metro)

Arsenal wampa kipaumbele cha kumsajili Fraser

Arsenal wanamtazamia winga wa klabu ya Bournemouth Ryan Fraser, 25, kama kipaumbele katika mipango yao ya usajili mwishoni mwa msimu. (Mirror)

Arsenal yaanza mazungumzo na Ituano kumsajili Martinelli

Klabu ya Arsenal ipo katika mazungumzo na klabu ya Brazil ya Ituano kwa usajili wa kitita cha pauni 6.5 milioni kwa winga kinda wa miaka 17 Gabriel Martinelli, ambaye amekuwa akifuatiliwa na vilabu vikubwa 20 vya barani Ulaya na hivi karibuni alifanya majaribio na Manchester United. (Sun)

Toure avishitumu vyombo vinayosimamia mpira

Kiungo wa zamani wa Manchester City Yaya Toure, 35, amevishutumu vyombo vinavyosimamia mpira wa miguu kwa kufeli kuwalinda wachezaji weusi dhidi ya ubaguzi. (Mirror)

Kocha Leicester kufanya mazungumzo na King

Kocha wa Leicester Brendan Rodgers anatazamiwa kufanya mazungumzo juu ya mustakabali wa kiungo Andy King, 30, klabuni hapo. (Leicester Mercury)

Howe apuuzia tetesi za Ake kusajiliwana vigogo EPL

Kocha Bournemouth Eddie Howe amepuuzia mbali tetesi kuwa klabu za Tottenham na Manchester United zinataka kumsajili beki wake Nathan Ake, 24.(Bournemouth Daily Echo)

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic