April 15, 2019


KOCHA mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kikosi chake kimeimarika tayari kwa ajili ya kubeba pointi tatu mkoani Morogoro, Jumatano mbele ya Mtibwa Sugar.

Yanga itashuka uwanjani, uwanja wa Jamhuri, Morogoro kumenyana na Mtibwa Sugar mchezo wa ligi wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo wa kwanza uliochezwa Taifa kwa mabao 2-1.

Zahera amesema kuwa hana cha kuhofia kwa sasa licha ya kuwakosa wachezaji wake muhimu wawili ambao ni Feisal Salum mwenye kadi tatu za njano na Kelvin Yondani mwenye kadi nyekundu.

"Najua utakuwa mchezo mgumu ila nimewaambia wachezaji wangu ni lazima tukashinde ili tujiweke sehemu nzuri ya kubeba ubingwa wa ligi hivyo ninaamini tutashinda ugenini kama ambavyo tumekuwa tukifanya mechi zilizopita.

"Kukosekana na Yondani na Feisal kwangu haina taabu sana tayari nimepata mbadala wao ambao wapo tayari kurejea kwa Abdallah Shaibu na Ibrahim Ajibu kunanifanya niwe na kikosi kipana, nina amini tutashinda," alisema Zahera.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic