April 15, 2019


Kiungo wa klabu ya Yanga SC, Feisal Salum Fei Toto na beki Kelvin Yondan wataukosa mchezo ujao wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar Jumatano ya April 17 kutokana na kuwa na kadi.

Toto ataikosa mechi hiyo kutokana na kuwa na kadi tatu ambazo kwa mujibu wa kanuni za soka hatopaswa kuwa sehemu ya mchezo.

Aidha, Kelvin Yondani ataukosa huo pia kutokana na kupigwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dhidi ya Kagera Sugar jijini Mwanza.

Wakati wawili hao wakikosekana, kikosi cha Yanga kinaondoka leo asubuhi kuelekea mjini humo kwa ajili ya mechi hiyo itakayoanza majira ya saa 10 kamili za jioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic