YANGA YAANZA KUIFANYIA UMAFIA SIMBA KWA MCHEZAJI WA KIMATAIFA
Wakati msimu wa Ligi Kuu Bara ukiwa unaelekea ukingoni kumalizika, imeelezwa kuwa mabosi wa Yanga wameanza jitihada mapema kufanya usajili wa maana ili kujipanga na msimu ujao.
Yanga imeanza mikakati hiyo wakiwa na jeuri ya kukusanya michango ya fedha kutoka kwa wanachama na mashabiki wa timu hiyo kutokana na harambee maalum waliyoiazisha hivi karibuni.
Taarifa za ndani kutoka Yanga ni kwamba mabosi wa timu hiyo wameshaanza harakati za kutaka kupata saini ya Jacques Tuyisenge ambaye ni mshambuliaji anayekipiga katika kikosi cha Gor Mahia FC ya Kenya.
Tuyisenge ambaye pia ilielezwa anawindwa na Simba, yupo kwenye rada ya Yanga hivi sasa tayari kabisa kutua ndani ya timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani, Kariakoo.
Simba walianza zamani kutajwa kutaka saini ya Tuyisenge lakini uongozi wao bado haujaweka hadharani suala hilo wakitaka kulifanya kimyakimya.
Uwezekano wa kipa huyo kutua hapa nchini upo ukizingatia timu yake ya Gor Mahia imekuwa ikipitia kipindi kigumu hivi sasa kwa kukosa fedha za kuiendesha pamoja na mishahara ya wachezaji kushindwa kulipwa kwa wakati.
Mwandishi kuwa makini tyuyisenge sio kipa
ReplyDeletetumekuchoka, maneno ya kijiweni haya
ReplyDelete