April 17, 2019


KIKOSI cha Yanga leo kimebanwa mbavu na Mtibwa Sugar kwa kufungwa bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, mkoani Morogoro.

Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera imepoteza mchezo wake wa nne kwenye ligi kuu hali inayofanya ishindwe kuonyesha ushujaa kwa kuipiga nje ndani Mtibwa Sugar na kukubali kuwa dhaifu ugenini.

Kwa mara ya kwanza Yanga msimu huu walianza kupoteza mbele ya Stand United mkoani Shinyanga, wakapoteza mchezo wao wa pili mbele ya Simba uwanja wa Taifa pia walipoteza mbele ya Lipuli uwanja wa Samora na leo mbele ya Mtibwa Sugar.

Bao la Mtibwa Sugar lilipachikwa kimiani na mshambuliaji Riphat Khamis dakika ya 52 baada ya kutumia makosa ya beki Abdalah Shaibu 'Ninja' na kuachia mkwaju nje ya 18 uliomshinda Klaus Kindoki.

Jitihada za Yanga kuibuka na ushindi hazikuzaa matunda kwani dakika ya 85 walipata bao kupitia kwa Amis Tambwe ambaye mwamuzi alionyesha kwamba ameotea akimaliza pasi ya Mrisho Ngassa.

Ushindi huu unaifanya Yanga kuendelea kusalia kileleni ikiwa na pointi 74 baada ya kucheza michezo 32, huku Mtibwa Sugar wakibeba pointi tatu na kufikisha jumla ya pointi 48.

12 COMMENTS:

  1. Zahera hafai anazidi kushuka ubora wake kutokana na matokeo haya!!!

    ReplyDelete
  2. Alidhaani ni akili mingi kuchezea Dar mechi 11 mfululizo na kwa ushindi wa 1-0 au 2-1 na bao LA kuongoza zaidi ya 60% ya mechi linapatikana baada ya dak 60!

    ReplyDelete
  3. TFF na waamuzi pia mnajenga imani kwa watanzania kuwa mnawaonea Yanga kwa kukataa magoli yao....ligi ya mwaka huu tutajionea mengi....nadhani katika ligi zote hii ya mwaka huu imetia fora!...kwa madudu....Simba kucheza mechi 7 ndani ya siku 17...hata Patrick Aussems amelizungumzia hili...kwakweli tunapoelekea kama nchi si pazuri....si ajabu hata Serengeti Boys kutolewa....yaani laana inaitafuna TFF.....

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wakati Yanga ilipokuwa inaiwakilisha taifa ilikuwa inapewa nafasi ya kutosha kujiandaa na michuano ya kimataifa...nao pia walikuwa na viporo..Viporo vya Simba vimekuwa vingi kwa sababu hawakuondolewa mapema tofauti na Yanga waliokuwa wanaondolewa mapema kwa miaka 4 mfululizo..Kusema kwamba Simba kutocheza kunaiathiri Yanga so kweli kwani tukio LA mechi za Yanga ni tofauti na LA mechi ya Simba na wala hayo matukio mawili hayategemeani!Mfano mzuri ni namna ilivyokuwa leo.Hivyo hata wakicheza muda mmoja kila timu inavuna inachopanda TFF wameshamjibu Zahera kuwa aondowe wasiwasi na acheze mechi zake..Katika siku 11 zinazofuata Simba itacheza mechi 5!Sasa kama Aussen angekuwa Zahera angelalamika kwamba hizo ni hujuma za kuinyima Simba ubingwa.Mechi za karibu karibu zinachosha wachezaji kiasi kwamba wanaweza wasifanye vizuri..Sio Yanga pekee inayoonewa...Simba pia inaonewa!

      Delete
    2. Kuna hoja kuwa wakati Yanga anawakilisha nchi hakuwa na viporo vinavyozidi 8+, nadhani tukubali ukweli kuwa Ligi yetu inatoa picha halisi kwanini hatufanikiwi katika mashindano ya kimataifa.....bado kuna Usimba na Uyanga....maamuzi mengi yanabase kwenye upenzi kuliko ukweli....TFF haiwezi kukwepa hizi lawama.....tunapoelekea si pazuri kwa mstakabali wa mpira wetu....

      Delete
  4. Zahera amesema kuwa sababu ya Yanga kufungwa Leo ni Muda wa saa nane.Kana kwamba Mtibwa wao wamecheza SAA kumi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hoja hii ya Zahera ni dhaifu....ila kiukweli ni kwamba ratiba ya mchezaji wa soka inapobadilikabadilika inaathiri utendaji wa kazi Mtibwa angeweza kushinda hata goli 3 kama mechi ingechezwa saw 10

      Delete
  5. Zahere kama kawaida yake kesho atalalamikia wameonewa na ubovu wa mpangalio wa mechi si rafiki ysoao na mengi mengineo

    ReplyDelete
  6. Viporo mwaka huu vimezidi pia kwa sababu msimu huu timu ni 20 na sio 16.Timu zimecheza mechi8 zaidi msimu huu.

    ReplyDelete
  7. Simba waligomea ligi kwny tofauti ya mech 4 za viporo na yanga mkumbuke alikua makund shirikisho, simba kavuka hatua moja toka makundi ambazo ni mech mbili, jiulizen smba ana viporo vngap sasa hv af kwa mech mbili tu za mazembe?

    ReplyDelete
  8. Jumlisha nä mechi 8 kwa sabdbu ligi ya mwaka huu kuna timu 20 sio 16 kama msimu uliopita.
    Pia msimu huu Yanga alianza na michezo 11 nyumbani baada ya,kukataa ratiba ya awali.

    ReplyDelete
  9. Shebby masaa 72 kabla ya Mechi ya TP ya Dar, Simba waliingia uwanjani Jamhuri kucheza na JKT mvua ikaharibu..Isingewezekana mechi kuchezwa Siku inayofuatia maana ingekuwa chini ya SAA 48 kabla ya Simba kucheza na TP Dar..Naona ulitaka mara baada ya mechi ya droo ya Dar ulitaka Simba icheze ligi baada ya SAA 72?Ndiyo na Zahere alitaka hivyo ili iwanufaishe wacongo wenzake was TP maana Simba angeingia kucheza amechoka..Hats Ten alitamani hivyo ili ile ndoto yake ya 8-0 itimie.Simba na TP wamerudiana baada ya siku 7 tu.Viporo vya Simba haviingiliani kabisa na matokeo ya Yanga.Na Zahera anapaswa kuuweka ukweli huo kwenye kona ya ubongo wake.Ila viporo vimeleta neema kwa Tanzania kwani vimesaidia Simba kufanya vizuri na sasa tuna timu 4 michuano ya kimataifa..hata wale Waliowashangilia Nkana na AS Vita kwa nguvu zote pale kwa Mkapa nao pia sasa watashiriki michuano ya kimataifa hata wasipofanikisha kupata Azam FA cup au ubingwa ligi kuu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic