April 17, 2019


Rais wa zamani wa Peru, Alan Garcia(69) amefariki baada ya kujipiga risasi kichwani leo Aprili 17, 2019 wakati Polisi walipofika nyumbani kwake katika Mji Mkuu wa Peru, Lima kumkamata kwa kumuhusisha na vitendo vya rushwa

Polisi walipowasili nyumbani kwake, alienda kujifungia chumbani kwake na kujipiga risasi, alikimbizwa katika hospitali ya Casimiro Ulloa na madakari walimfanyia upasuaji wa dharura lakini saa kadhaa baadaye alifariki

Awali, Shirika moja la habari la nchini humo lilitoa taarifa kuwa Garcia alikuwa katika hali mahututi huku likionesha picha za mtoto wa Rais huyo, Watu wanaomuunga mkono na Wabunge wakiingia hospitalini na Polisi wakiwa wamezingira hospitali

Rais huyo wa zamani alikuwa anachunguzwa akihusishwa na Kampuni ya Ujenzi ya Brazil, Odebrecht ambayo mwaka 2016 ilikiri hadharani kuwa ilishinda mikataba yenye faida kubwa ya ujenzi kwenye ukanda wa Amerika ya Kusini kwa kuhonga

Huku mara zote akikataa kuhusika na kufanya makosa yoyote, mwaka jana Garcia aliomba hifadhi nchini Uruguay baada ya kuzuiwa kuondoka Peru kwa kuwa uchunguzi dhidi yake unaendelea, lakini Uruguay ilikataa ombi hilo

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic