April 17, 2019


SIMBA iliyo chini ya Kocha Mkuu Patrick Aussems, leo kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu Bara wamepindua meza kibabe baada ya kufungwa mapema na Razini Hafidh wa Coastal Union akimalizia mpira uliowachanganya wachezaji wa Simba, Aish Manula ambaye ni mlinda mlango na beki Erasto Nyoni dk ya 01.

Bao hilo lilidumu mpaka kipindi cha pili ambapo Simba walianza kuwanyua mashabiki dakika ya 49 kwa mkwaju wa penalti baada ya mchezaji wa Coastal Union kumchezea rafu Emanuel Okwi ndani ya 18 iliyozamishwa kimiani na Meddie Kagere.

Simba waliendelea kuonyesha utofauti wao licha ya kucheza kwenye uwanja wa Mkwakwani ambao ni kipara kwa kuwa hakuna majani sehemu kubwa ya uwanja na dakika ya 68 Kagere alirejea tena nyavuni akimaliza pasi mpenyezo ya Clatous Chama na kupachika bao la pili na la ushindi.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 60 baada ya kucheza michezo 23 huku wakisalia kwenye nafasi yao ya tatu kwani kinara ni Yanga mwenye pointi 74 ambaye amecheza michezo 32.

Kwa msimu huu ni mara ya kwanza Simba kupindua matokeo kwani mchezo wa kwanza kupoteza walianza kufungwa na Mbao FC msimu uliopita dk ya 16 na Said Junior bao lililodumu mpaka dakika ya 90 Uwanja wa CCM Kirumba.

4 COMMENTS:

  1. Kituo kinachofuata 🤷‍♂️🤷‍♂️🤷‍♂️

    ReplyDelete
  2. TFF na waamuzi pia mnajenga imani kwa watanzania kuwa mnawaonea Yanga kwa kukataa magoli yao....ligi ya mwaka huu tutajionea mengi....nadhani katika ligi zote hii ya mwaka huu imetia fora!...kwa madudu....Simba kucheza mechi 7 ndani ya siku 17...hata Patrick Aussems amelizungumzia hili...kwakweli tunapoelekea kama nchi si pazuri....si ajabu hata Serengeti Boys kutolewa....yaani laana inaitafuna TFF.....

    ReplyDelete
  3. Yanga akishinda mechi zake 6×3=18+74=92.....simba....15×3=45+ 60 itafikia point 105.....gap la points kila mtu akishinda mechi zilizobaki....105-92=13

    Hivi hata Yanga ingepewà hill goli feki! Ingepata point moja ambayo haitaifikisha popote!

    ReplyDelete
  4. MATUMAINI YA KUOMBEA MWENZIO MABAYA NDIPO UPITE MIE SIYAAMINI YANGA TUSHAKWISHA HAIJAWAHI TOKEA HIVI KARIBUNI TIMU IFUNGWE MICHEZO 4 HALAFU AWE BINGWA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic