YONDANI AFUNGIWA MECHI TATU NA KUTOZWA FAINI YA LAKI TANO
Mchezaji Kelvin Yondani wa Yanga amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya shilingi 500,000 (laki tano) baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa Kagera Sugar FC katika mechi hiyo iliyochezwa Aprili 11, 2019 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 38 (9) ya Ligi Kuu Toleo la 2018 kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.
Ohh basi huyu ni boxer sio football player.
ReplyDelete