April 23, 2019


Naomba radhi kwa post kama 20 ambazo zimekukwaza kwa njia moja au nyingine ,sababu hazikuwa post zenye busara na hekima.

Nimepata dhamana kubwa sana na heshima kuwa msemaji wa club kubwa nchini Tanzania,Young African na sipo tayari kuharibu heshima yangu pamoja na taswira ya club yangu.

Kuna mtu ambaye ametumia vibaya account hii,bila kujali heshima,busara na utu wa rika la watu wanaopenda kujifunza na kusikia taarifa muhimu kuhusu club yetu na mambo ya msingi.

Naombeni radhi ,mnisamehe na kunipa nafasi nyingine ili niweze kusafisha pale nilipochafua .

Kazi yangu inahitaji usafi wa kinywa ,maandishi na weredi ,nitajitahidi sana kutorudia kosa na kutumia zaidi maarifa ,haki na ushujaa.

Na Dismas Ten

5 COMMENTS:

  1. acha kutuchezea akili, post hizo hazijatumwa kwa siku moja, nyingine zinapishana hadi wiki. kwa nini ulikuwa kimya? ulidhamiria kuandika hivyo.

    ReplyDelete
  2. Huo ndio uwezo wako wa kufikiri.Ksma akaunti ilichezewa kwanini uombe radhi?Post 20 ukurupuke leo
    Au kuna jamaa wa Yanga wameudhika na ujinga wako hivyo umelazimika kuomba radhi??

    ReplyDelete
  3. Huyo kupost hata matusi ni kawaida.. Luna jamaa alimbishia mtandaoni akaishia kumtukania mama yake

    ReplyDelete
  4. Halafu ndio msemaji wa mapoyoyo. Akizidiwa hoja lazima uoge matusi ya nguoni.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic