April 18, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ni kama ameishtaki Simba kwa Shirikisho la Soka Afrika (Caf), baada ya kukutana nao na kuwaeleza namna ambavyo wapinzani wao hao walivyokuwa na viporo vingi katika Ligi Kuu Bara.

Simba ambayo leo Jumatano inapambana na Coastal Union, ina mechi 16 mkononi kabla ya kumaliza msimu huu wa Ligi Kuu Bara, huku Yangaambayo nayo inacheza na Mtibwa Sugar leo, ina mechi saba.

 Tofauti ya mechi za Simba na Yanga ni tisa kitu ambacho Zahera anaamini kinaweza kuifanya Simba kuwa bingwa kirahisi kutokana na kuwa na mechi nyingi mkononi zaidi yao licha ya kwamba wao wanaongoza ligi kwa sasa.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Yanga ikiwa imecheza mechi 31, inaongoza ikiwa na alama 74, huku Simba ikicheza mechi 22, inashika nafasi ya tatu na alama zake 57.

Hivi karibuni, Zahera alikutana na viongozi wa Caf ambao kwa sasa wapo jijini Dar wakifuatilia michuano ya vijana ya Kombe la Mataifa Afrika chini ya miaka 17 na kuwaeleza jambo hilo.

“Nilikutana na viongozi wa Caf wale waliokuja kwa ajili ya Afcon U-17, wakaniuliza namna gani tunaendelea na ligi, nikawaambia kuna timu moja hapa ina mechi 16 bado haijacheza na zingine zina mechi tano mpaka sita, walicheka sana,” alisema Zahera ambaye ni raia wa Ufaransa na DR Congo.

Ishu ya Simba kuwa na viporo vingi imetokana na kushiriki kwao michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo wikiendi iliyopita waliondoshwa hatua ya robo fainali.

4 COMMENTS:

  1. Huyu Zahera sifikiri kama anakijuwa anachokisema au kukilalamikia. Juu ya kufungwa na kutoka droo katika mechi kadhaa, yeye bado yumo lazima anataka ubingwa uwe wake na hakifahamiki anachokisema. Huenda anataka itambulike kuwa yanga imeonewa na iamuliwe ubingwa utangazwe mapema wa yanga.

    ReplyDelete
  2. huyu jamaa hatufai CAF wanfanya kazi na TFF moja kwa moja

    ReplyDelete
  3. Alishaona hawezi pata tena kombe kwa kucheza dakika 90 uwanjani..sasa analitafuta kwa malalamiko na mashitaka..kila LA heri Zahera

    ReplyDelete
  4. Mropokaji tu huyo .Timu yetu imekuwa butua butua.
    Hamna plan B.
    Tunamvumilia kwa sababu hamna namna. Ukata.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic