UONGOZI wa Azam FC, umesema kuwa kwa sasa wanajipanga kumtafuta mchezaji mwingine ndani ya kikosi hicho atakayeziba nafasi ya kiungo mshambuliaji, Tafadzwa Kutinyu ambaye amejiunga na kikosi cha Horoya AC ya Guinea.
Ofisa Habari wa Azam FC, Jafary Maganga amesema kuwa mkataba wa mchezaji huyo unameguka mwisho wa msimu huu hivyo hawana tatizo naye kwa kuwa anakwenda kutafuta maisha sehemu nyingine.
"Mchezaji wetu Kutinyu mkataba wake unamalizika mwisho wa mwezi huu, tumeadikiwa barua na chama cha Soka cha Zimbabwe wakimhitaji Kutinyu kwa ajili ya mashindano ya COSAFA kwa hiyo kwa sasa yupo Zimbabwe.
"Hatutakuwa naye tena Azam FC msimu ujao na anatupa nafasi ya kumtafuta mchezaji mwingine ambaye atachukua nafasi yake, yeye ni mchezaji huru ana nafasi ya kwenda pale anapotaka kwenda hatua mashaka kila kitu kitakuwa sawa," amesema.
Jembe limeenda kungana na jembe kutoka Yanga ambaye ni Makambo aka HM 19.Mungu awatangulie huko muendako.
ReplyDelete