May 30, 2019


Uongozi wa klabu ya Yanga umemalizana na beki Lamine Moro kwa kusaini mkataba wa miaka miwili.

Moro ambaye ni raia wa Ghana, ambaye aliwahi kuja Simba kufanyiwa majaribio kipindi cha michuano ya SportPesa CUP, amefikia mwafaka kwa kusajiliwa na Yanga.


Beki huyo sasa atakuwa Jangwani mpaka mwaka 2021 akiihudumia timu hiyo ambayo ni bingwa wa kihistoria katika Ligi Kuu Bara.

Usajili huo unafanyika ikiwa ni jithada za Yanga kuongeza nguvu ndani ya kikosi chao tayari kwa maandalizi ya kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

5 COMMENTS:

  1. Beki Simba....alisajiliwa lini na Simba?

    ReplyDelete
  2. Jifunzeni kuandika kichwa cha habari hakiendani na habari yenyewe

    ReplyDelete
  3. Duh usajili unaoendelea mitaa ya Jangwani ni balaa hii inaitwa "Yanga Kubwa Kuliko" wengine wanaiita "Yanga Mabadiliko" au "Yanga Yenye Kasi Mpya

    ReplyDelete
  4. kwa jinsi alivyocheza SportPesa Super Cup...Jamaa ni bonge la beki

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic