May 9, 2019


MAMBO ni mengi muda ni mchache! Unaambiwa huko Insta kumechafuka, watu wako bize kwelikweli, wanaijadili bodaboda aliyopewa Miss Mbeya, Angela Deocress hivi karibuni. 

Kwenye maoni mbalimbali waliyochangia wadau wa mtandao huo, wapo walioponda lakini pia wapo waliosema ni sawa tu mrembo huyo kupewa bodaboda.

“Tuangalie na hali halisi ya biashara kwa sasa, kumpa mrembo gari ni kuamua kujitolea bila kupata faida na zaidi utumie pesa yako ya pembeni.

"Makampuni yamefilisika mengi na udhamini ni mgumu. Mimi binafsi naona ni bora warembo wapewe pesa taslimu kuliko vitu,” aliandika Firstladyafrica na kuungwa mkono na wengine kibao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic