May 9, 2019



Yanga wanadai kupoteza dhidi ya Lipuli FC ya Iringa katika mchezo wa FA, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)  ndio chanzo kutokana na kukataa kubadilisha ratiba.
 Yanga ilipokea kipigo cha mabao  2 -0 dhidi ya Lipuli katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Samora, Iringa katika mchezo wa FA.


Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa, kuwepo kwa mambo mawili katika klabu yao ndio kumewagharimu kuweza kupoteza mchezo huo.
“Kitu kilichotugharimu kupoteza mchezo na Lipuli ni kuwa na mambo makubwa mawili kwa wakati mmoja ikiwemo lile la uchaguzi na hili la mchezo wetu wa FA ambao hatukuweza kufanya maandalizi mazuri kutokana na uchaguzi.


“Tuliwaomba TFF waweze kusogeza mbele mchezo huu lakini walitukatalia hivyo matokeo yamekuwa haya na Wanayanga wote wamekubaliana na matokeo hivyo tunajipanga zaidi kwa ajili ya msimu ujao.


“Tunahitaji kukamilisha mechi zetu za ligi zilizobakia kwa kuhakiksha tunashinda huku tukijipanga kwa ajili ya msimu ujao,” alisema Mwakalebela ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa TFF na kuongeza:


“Unapokuwa na mambo makubwa mawili mazito moja lazima litakuzidi  nguvu, ilitumika nguvu zaidi kwenye uchaguzi,” aliongeza.


3 COMMENTS:

  1. Visingizio mmeanza na ugeni wenu?Simba alifanya mkutano Dar na kucheza Tanga na JKT siku hiyo hiyo.Na wakashinda 2 bila.
    Kwani mechi ya pili na Lipuli tulikuwa na mkutano? Tuache visingizio Lipuli walituzidi uwezo .

    ReplyDelete
  2. Acheni unafiki!sasa mbona mlikuwa mnashinikiza Simba icheze premium ligi na CAF kwa wakati mmoja?Kumbe mnajua madhara ya kufanya mambo mawili makuu kwa wakati mmoja huleta gharama kwa mojawapo!Halafu unasikia eti Simba wanapendekewa na viporo ni kuwatayarishia ubingwa!Kweli TFF kwa busara zao wameipangia Simba mechi 7 katika siku 16.Wote tunajua madhara ya kuingia uwanjani ukiwa na uchovu!Nini kimewakuta Coastal jana!Hongera kocha Aussens kwa kutumia rotation ya Wachezaji!Ni hicho tu ndiyo kinaisaidia Simba...Leo Niyonzima anacheza na mechi ifuatayo anapumzishwa au kuingia kama sub muda ukiwa umeenda

    ReplyDelete
  3. Hahaha hatariii sana...mpira sio siasa jamani dah..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic