BOSI SIMBA ATOA TAMKO JUU YA KAGERE KWENDA ZAMALEK
Uongozi wa klabu ya Simba umesema hamna ofa yoyote iliyotolewa na timu yoyote ile juu ya mshambuliaji wao hatari, Meddie Kagere.
Licha ya tetesi kuibuka hivi karibuni zikieleza kuwa Kagere amekuwa akiwindwa na klabu kadhaa ikiwemo Zamalek ya Misri, Ofisa Mtendaji wa Simba, Crescentius Magori, amekanusha taarifa hizo.
Magori amesema hawana ofa yoyote iliyofika mezani kwa ajili ya Kagere kutakiwa na badala yake wamekuwa wakisikia stori ambazo si rasmi.
Ameeleza kama wana nia ya kumtaka Kagere walete ombi lao kwa maandishi na waweze kukubaliana juu ya usajili wa straika huyo.
"Hakuna ombi lolote lililokuja mezani kuhusiana na Kagere kusajiliwa Simba.
"Ni taarifa tu za mitandaoni ambazo si rasmi zimekuwa zikiandikwa.
"Kama wapo SIRIAZI na wanamtaka mchezaji, si Zamalek tu hata wengine, wanapaswa kuja na tutazungumza na si matamko ya mitaani huko."
0 COMMENTS:
Post a Comment